Home » » MTOTO WA MIAKA 8 AFARIKI BAADA YA KULIPUKIWA BOMU MKONONI

MTOTO WA MIAKA 8 AFARIKI BAADA YA KULIPUKIWA BOMU MKONONI



Na Emmanuel J Matinde(Kigoma yetu Blog)
KIGOMA
Wednesday June 6, 2012

Motto mwenye umri wa miaka 8 mwanafunzi wa darasa la kwanza Obeid Manase mkazi wa kijiji cha Kigadye wilayani Kasulu mkoani Kigoma amefariki dunia baada ya bomu la kutupwa kwa mkono alilokuwa akichezea na wenzake kulipuka 
Kamanda wa polisi mkoani Kigoma kamishina msaidizi wa polisi Frasser Kashai amesema tukio hilo limetokea Juni sita mwaka huu majira ya saa kumi na moja jioni katika kijiji cha Kigadye kata ya Herushingo tarafa ya Makere wilayani Kasulu mkoani Kigoma
Amesema watoto watano walikuwa wakilichezea bomu hilo na kuwalipukia na kusababisha kifo cha mmoja wao ambaye alifariki papo hapo na wengine wanne kujeruhiwa
Amewataja watoto waliojeruhiwa katika tuko hilo kuwa ni Tuju Seluke(7), mwanafunzi wa darasa la kwanza aliyejeruhiwa tumboni, Angel Seluke (4) ambaye alijeruhiwa sikio la kushoto, Sarah Manase(6) aliyejeruhiwa paja la kulia na Isaack Yohana(4) aliyejeruhiwa jicho la kushoto ambao wote wamelazwa katika hospitali ya Heri Mission wilayani Kasulu na hali zao zinaendelea vizuri.
Akizungumzia bomu hilo lililosababisha kifo cha motto huyo kamanda Kashai amesema uchunguzi uliofanywa na jeshi la polisi umebaini kuwa watoto hao walilichukua bomu hilo kwenye maua sehemu inayoaminika kuwa lilifichwa na baba yake mdogo na marehemu aitwaye Ayub James na Juhudi za kumtafuta kwa mahojiano zinaendelea.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa