Home » » WAHAMIAJI HARAMU 52 WAKAMATWA KIGOMA

WAHAMIAJI HARAMU 52 WAKAMATWA KIGOMA


Na Emmanuel J Matinde(Kigoma yetu Blog)
KIGOMA
Wednesday June 6, 2012

Jumla ya watu 52 wanaodaiwa kuwa wahamiaji haramu wamekamatwa katika maeneo mbali mbali mkoani Kigoma ambao ni raia wan chi za Burundi na Congo DRC ambao wengi wao wamekuwa wakifanya shughuli za uvuvi katika maeneo ya Katonga mkoani humo
Kamanda wa polisi mkoani Kigoma kamishina msaidizi wa polisi Frasser Kashai amesema juhudi za kuwakamata wahamiaji hao haramu zimefanywa na jeshi la polisi kwa kushirikiana na idara ya uhamiaji mkoani Kigoma kufuatia msako uliofanyika kati ya mei 25 na Juni 5 mwaka huu.
Amesema kati ya waliokamatwa 14 tayari wamefikishwa mahakamani huku wengine wakiendelea kufanyiwa uchunguzi na maafisa wa idara ya uhamiaji
Katika hatua nyingine jeshi la polisi mkoani Kigoma linawashikilia watu sita kwa tuhuma za kukutwa na madawa ya kulevya aina ya bangi kilo 18
Kamanda wa Kashai amewataja watu hao kuwa ni Sued Said mkazi wa Masanga Kigoma, Kassim Dibwili mkazi wa eneo la SIDO Kigoma na Mdasimzi Madua na Amani Abdul wakazi wa Mwadui.
Wengine ni Rubone Yasin na Karanga Mahamu wote wakazi wa Mwandiga na kwamba watuhumiwa wote sita walikamatwa mei 25 mwaka huu majira ya tisa alasiri eneo la SIDO manispaa ya Kigoma Ujiji.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa