Home » » SERIKALI YA TANZANIA YAOMBWA KUSAIDIA KUIMARISHA USALAMA NCHIN ZA MAZIWA MAKUU

SERIKALI YA TANZANIA YAOMBWA KUSAIDIA KUIMARISHA USALAMA NCHIN ZA MAZIWA MAKUU


Na Emmanuel J Matinde-Kigoma yetu
KIGOMA 
Thursday June 21, 2012
Serikali ya Tanzania na shirika la kuhudumia wakimbizi ulimwenguni UNHCR zimeombwa kusaidia kuimarisha usalama na amani katika nchi za maziwa makuu ili wakimbizi waishio uhamishoni warejee nchini mwao
Mwenyekiti wa kambi ya wakimbizi ya Mtabila iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma bw.Silvester Benjamini amesema ametoa ombi hilo hapo jana katika maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani
Akisoma risala katika maadhimisho hayo bw.Benjamini amesema wakimbizi wote wako katika mchakato wa kurudi nchini mwao kutokana na kwamba hali ya amani imeimarika na kwamba wasingependa kuona hali ya vita ikirejea tena nchini Burundi
“Tunaiomba serikali ya Tanzania kuendelea kusaidia nchi za maziwa makuu ikiwemo Burundi kuendelea kuwa na amani ili turejeapo kwetu tuweze kujivunia mwendelezo wa amani iliyopo nchini Burundi kwa sasa,alisema bw.Benjamaini. 
Aidha ameishukuru serikali ya Tanzania kwa kuwapa hifadhi kwa zaidi ya miaka kumi na sita wakiwa kama wakimbizi ikiwa ni pamoja na mashirika yote yanayotoa huduma mbali mbali tangu walipoyakimbia makazi yao kutokana na vita ya wenyewe kwa wenyewe huko nchini Burundi.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa