Home » » VIONGOZI WA KIJIJI NA KATA WATUHUMIWA KWA UFISADI – KIGOMA

VIONGOZI WA KIJIJI NA KATA WATUHUMIWA KWA UFISADI – KIGOMA


Na Emanuel- Kigoma yetu
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Nyarubanda kata ya Mkigo wilayani Kigoma wametoa malalamiko yao dhidi ya viongozi wa serikali ya kijiji chao kwa kushindwa kutoa taarifa ya mapato na matumizi kwa baadhi ya miradi ya maendeleo ya kijiji
Wakiongea na kituo hiki kwa nyakati tofauti wananchi hao wamewashutumu mwenyekiti wa kijiji cha Nyarubanda bw.Thobiasi Bichulo na diwani wa kata ya Mkigo bw.Said Betese kwa kukosa uadilifu na kutumia mali za kijiji hicho kujinufaisha wenyewe
Mmoja wa wananchi hao bw.Uledi Kamenya amesema wananchi walihoji suala hilo katika mkutano wa hadhara uliofanywa na diwani wa kata ya Mkigo bw.Betese mwaka jana na tume ikaundwa kuchunguza suala hilo na kubainika wizi wa bati 180 lakini hakuna hatua zilizochukuliwa
“Tarehe mbili mwezi wa nane mwaka jana tulihoji kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa na mheshimiwa diwani ikalazimika kuundwa kwa tume na baada ya kuundwa kwa tume ikaonekana kuna wizi wa bati 180 uliofanyika High school Nyarubanda, cha kushangaza sasa mheshimiwa huyo huyo diwani amekuwa akitoa rushwa kwa askari polisi ili waweze kuwakamata wananchi wanaohoji mali za umma ili kuwafunga midomo, alisema Kamenya.
Aidha amesema mwaka 2006 serikali ilitoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya mwalimu lakini kwenye tume hiyo iliyosimamiwa na mheshimiwa diwani ilionesha kwamba nyumba imejengwa wakati nyumba haionekani mpaka leo 
Nae bw.Matheo Rugasila amesema maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya huduma za umma yanavamiwa lakini mwenyekiti wa serikali ya kijiji bw.Bichulo ameshindwa kuyashughulikia hali inayoibua mashaka kwa wananchi kuwa huenda yanauzwa kinyemela
Juhudi za kumtafuta mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Nyarubanda bw.Thobias Bichulo kuzungumzia suala hilo ziliishia kumpata kwa njia ya simu ambapo alikanusha kwamba hakuna kitu kama hicho huku diwani wa kata ya Mkigo bw.Said Betese yeye akikataa kutoa ushirikiano.
Hata hivyo taarifa ambazo zimepatikana zimedain kuwa suala la madai ya wananchi hao dhidi ya viongozi wao liko mahakamani ili hatima yake iweze kujulikana.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa