Home » » DOLA BANDIA ZAWAKAMATISHA WATU WAWILI

DOLA BANDIA ZAWAKAMATISHA WATU WAWILI

Na Editha Karlo, Kigoma
JESHI la Polisi mkoani Kigoma linawashikilia vijana wawili kwa kosa la kukutwa na noti bandia za Dola 200 za Marekani zenye namba AL 05972343 CL12 na AL 05972343 CL12.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kigoma, Frasser Kashai, aliwataja watuhumiwa hao ambao ni wakazi wa Gungu kuwa ni Ally Hassan (27) na Jumanne Sudi (19).

Alisema vijana hao walikamatwa na askari polisi waliokuwa katika doria ya usiku katika eneo la Mwanga Madukani, wakiwa katika harakati za kubadilisha fedha.

Alisema vijana hao walikwenda Mwanga katika duka la mfanyabiashara mmoja kwa nia ya kubadilisha fedha za kigeni.

Alisema baada ya mfanyabiashara huyo kupokea dola hizo alizishitukia kuwa ni bandia, ndipo alipotoa taarifa kwa askari waliokuwa doria katika eneo hilo na kufanikiwa kuwakamata na kuwapeleka kituo cha polisi.

Katika tukio jingine, wakazi wa Kijiji cha Nyenge wilayani Kasulu, Moses Reuben (29) na Dotto Verimana (18) wanashikiliwa kwa kosa la kuhusika katika mauaji ya Moshi Pagota (48).

Alisema chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi uliosababishwa na ulevi wa pombe za kienyeji walizokunywa pamoja. Watuhumiwa wanatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote upelelezi utakapokamilika.
Chanzo: Mtanzania

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa