Na Editha Karlo, Kigoma
WIZARA ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), imefanikiwa kumaliza mgogoro wa ushuru kati ya uongozi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji na wafanyabiashara.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara baada ya kikao na Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Naibu Waziri wa TAMISEMI, Agrey Mwanri, ameitaka manispaa kufanya uchambuzi wa viwango vya kodi na ushuru na kutowatoza ushuru wafanyabiashara ndogo ndogo kama taratibu za Serikali zinavyotaka.
Alisema kutoza ushuru kwa wafanyabiashara wanaofanya biashara ndogo ndogo kwa ajili ya kujikimu kama vile biashara ya mchicha na vitumbua hiyo ni kama kero kwa wafanyabiashara hao, hivyo Serikali iliamua kufuta ushuru huo na kuamua kutoa ruzuku kwa halmashauri tangu mwaka 2003.
Kwa upande wao, wafanyabiashara wa Manispaa ya Kigoma Ujiji wamelalamikia kitendo chao cha kupandisha ushuru kwa asilimia 100 bila ya kuboresha miundombinu katika masoko.
“Kwa kweli sijui kwa nini ushuru wametupandishia kwa asilimia 100, lakini miundombinu ya soko bado haijaboreshwa hata kidogo, ukiangalia hali ya vyoo ni mbaya, soko ni chafu, sasa sijui hizo fedha wanazotoza za ushuru zinakwenda wapi na kufanya nini,” alihoji Rehema Hamis ambaye ni mfanyabiashara wa Soko la Nazareth.
Mgogoro huo wa kupanda kwa ushuru kwa asilimia 100 pamoja na kuwatoza wafanyabiashara wadogo ushuru kinyume na taratibu, umedumu takriban mwezi mmoja na ulisabaisha wafanyabiashara kugoma na wakati mwingine uongozi wa manispaa kufunga masoko yake.

Chanzo: Mtanzania
0 comments:
Post a Comment