Na Rose Mweko, aliyekuwa Kasulu
SERIKALI imeshauriwa kuacha kubadili mitaala mara kwa mara na hatimaye kuwawezesha wanafunzi kuelewa na kufaulu masomo yao.
Wakizungumza na MTANZANIA kwa nyakati tofauti wilayani Kasulu, baadhi ya walimu walisema kubadilisha mitaala kunawafanya walimu na wanafunzi kutofanikiwa na kuwa na ufaulu unaotakiwa.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Tulieni, Bakari Maulidi, aliiomba Serikali kutobadili mitaala, kwa kuwa kufanya hivyo kutasababisha masomo ya wanafunzi kushuka.
“Mitaala inapobadilika inabidi na vitabu vibadilike na hata walimu wanatakiwa kupelekwa semina kuendana na mabadiliko ya mitaala, jambo ambalo ni gharama kubwa kwa Serikali na pia inawagharimu wanafunzi kutoweza kujipanga vizuri kimasomo, hasa wale wanaokuwa mwaka wa mwisho,” alisema Bakari.
Naye, Mwalimu Siasa Selemani wa Shule ya Msingi Kabanga, alisema shule nyingi wanalalamikia kuwa na uhaba wa vitabu, si kwamba vitabu vinakuwa havipo, ila kutokana na kubadilika kwa mitaala vitabu ambavyo vilinunuliwa katika msimu uliopita vinakuwa havina kazi kwa msimu huo.
“Kwa mfano, ndani ya miaka hii mitano kumeshabadilika mitaala kama mara tatu ambapo tunakuwa tayari tumeshanunua vitabu, unadhani tutavipeleka wapi na tutapata wapi fedha za kununua vitabu vingine, hii inatuwia vigumu hata kwa walimu katika ufundishaji,” alisema Selemani.
Aidha, alisema mitaala inapobadilika walimu hawapelekwi semina na matokeo yake wanapelekwa wataalamu walioko katika ofisi za halmashauri, wakati wao hawafanyi kazi za kuwafundisha watoto.
“Mara nyingi mitaala inapobadilika halmashauri huwachukua wakaguzi na wakuu wa idara na kuwapeleka katika semina za mabadiliko ya mitaala, walimu wanajiuliza kwamba wao ndio wanaokwenda kuwafundisha watoto, iweje wapelekwe hao wengine,” alisema Selemani.
Aidha, Mwalimu wa Shule ya Msingi Katoto, Issa Ntabhindi, aliitaka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kutowadharau walimu na kubadili mitaala kutokana na maslahi yao binafsi, kwa kuwa kufanya hivyo wanaendelea kuiua elimu ambayo hadi sasa inaelekea kufa.
“Malalamiko ya walimu mara zote yapo kwa aina nyingi, pamoja na kulalamikia maslahi, lakini pia waangalie na namna wanavyobadili mitaala kutokana na uroho wa asilimia 10,” alisema Ntabhindi.

Chanzo: Mtanzania
0 comments:
Post a Comment