Na Editha Karlo, Kigoma
JESHI la Polisi mkoani Kigoma linawashikilia watu wawili Fortness Samweli na Nika Samweli, wote wakazi wa Mtaa wa Mwasenga kwa tuhuma za kumfunga kamba mikononi, kumfungia ndani na kumnyima chakula kwa siku tatu mfululizo mtoto Rela Bonifasi (8).
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Fraisser Kashai, alisema mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili katika Shule ya Msingi Mwasenga, kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Kigoma, akiendelea na matibabu ya majeraha aliyoyapata.
Alisema chanzo cha mtoto huyo kupatwa na mateso hayo ni baada ya kwenda kuoga katika Mto Mungonya, nje kidogo ya mji wa Kigoma na baada ya kutoka kuoga mama yake mzazi na mjomba wake walishirikiana kumpiga na kumfunga kamba mikononi.
Alisema majirani wema ndio waliotoa taarifa polisi baada ya siku tatu kutomuona mtoto huyo, ndipo wakaingiwa na shaka na kutoa taarifa polisi na walipokwenda nyumbani kwa mtuhumiwa na kukuta mtoto kafungiwa ndani huku akiwa na majeraha.
Alisema washitakiwa wote wawili wameshakamatwa na watafikishwa mahakamani wakati wowote baada ya uchunguzi kukamilika.
MTANZANIA lilikwenda katika hospitali hiyo na kumshuhudia mtoto huyo akiendelea na matibabu katika wodi namba saba, huku akiwa na majeraha.
Akizungumza kwa tabu, mtoto huyo alisema amesikitika kitendo alichofanyiwa na mama yake mzazi na mjomba wake.
Alisema kutokana na mateso hayo amepata majeraha sehemu za mapajani na mikononi na kutokana na kufungwa kamba kwa muda wa siku tatu na imekufa ganzi na hawezi kushika kitu bila ya msaada.
Baadhi ya akina mama waliozungumza na Mtanzania wamelaani kitendo hicho.
“Sisi wote ni wazazi ila kwa kweli hakuna adhabu ya hivyo kwa mtoto ule ni unyama na ukatili mkubwa. Tena anayemfanyia vile ni mama yake mzazi hapo lazima sheria ichukue mkondo wake na iwe fundisho kwa wale wote wanaowanyanyasa watoto,” alisema Halima Rashidi.

Chanzo: Mtanzania
0 comments:
Post a Comment