Home » » SERUKAMBA APINGA USHURU KWA MAMA LISHE

SERUKAMBA APINGA USHURU KWA MAMA LISHE

JIBU LA SWALI LA MBUNGE Kigoma mjini

na Mwandishi wetu, Dodoma
MBUNGE wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba (CCM), ameitaka serikali itoe kauli yake bungeni juu ya baadhi ya halmashauri nchini ambazo zinaendelea kuwatoza ushuru kina mama lishe na wafanyabiashara ndogo ndogo.
Mbunge huyo alitoa kauli hiyo jana bungeni wakati alipokuwa akiuliza swali la papo kwa papo kwa Waziri Mkuu.
Alitaka kujua kauli ya serikali pamoja na kutangaza kufuta ushuru huo kwa maana ya kupatiwa ruzuku kwa ajili ya maendeleo.
Vile vile mbunge huyo alimtaka Waziri Mkuu kutoa tamko juu ya Meya wa Manispaa ya Kigoma Mjini kufunga masoko yote kwa ajili ya kudai ushuru ambao tayari serikali ilishauzuia.
Akijibu swali hilo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema kuwa ni kweli serikali iliishapiga marufuku ukusanyaji wa ushuru kwa wafanyabiashara ndogondogo ili waweze kupata faida.
Hata hivyo Pinda alisema kutokana na tuhuma za mbunge kumshutumu meya kwa ajili ya kufunga masoko, serikali ipewe muda kwa ajili ya kulishughulikia jambo hilo kwa ufasaha.
Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa