na
Mwandishi wetu, Kigoma
BENKI
ya Exim imeendelea kupanua huduma zake nchini kwa kuzindua tawi jipya mkoani
Kigoma, ikiwa ni jitihada za kuwafikishia huduma za kibenki wananchi wengi
zaidi nchini.
Tawi
hilo jipya litakuwa la 23 nchi nzima huku benki hiyo ikiwa imethubutu kufungua
matawi mengine mawili nje ya nchi yakiwa nchini Comoro na Djibouti.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa tawi hilo, Mkurugenzi wa benki hiyo, Hanif Jaffer,
alisema ufunguzi wa tawi hilo ni utekelezaji wa mpango wa benki unaolenga
kuhakikishia wananchi wengi wanapata huduma bora za kibenki.
Jaffer
alisema benki yake imeamua kufungua tawi hilo kutokana na ukweli kuwa Mkoa wa
Kigoma ni kiungo muhimu kwa wananchi wanaofanya biashara na nchi jirani za
Burundi na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo.
Alisema
kuwa benki yake itaendelea kuwapatia wajasiriamali wadogo na wakati uwezo wa
kifedha ili kuwasaidia kupanua biashara zao.
“Jitihada
zetu ni kuhakikisha tunafikia wananchi wengi waliopo pembezoni. Tuna imani kuwa
ufunguzi wa tawi letu jipya hapa litasaidia kupunguza tatizo hilo,” alisema
Jaffer.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment