Na, Mwandishi Wetu, Kigoma.
IMEBAINIKA kuwa Halmashauri ya Manispaa Kigoma Ujiji imetawaliwa na mchwa watafuna fedha za walipa kodi kwa maslahi yao binafsi.
Hayo yamebainishwa na Katibu Mwenezi wa NRA Taifa Hamisi Kiswaga wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Buzebazeba katika Manispaa ya Kigoma ujiji ambapo halimashauli hiyo inashutumiwa kwa ubadhilifu wa fedha bila kujali maendeleo ya wananchi waliowachagua kwa mujibu wa taarifa ya mkaguzi mkuu wa fedha Mkoani hapo.
“watumishi wengi wa serikali hawana uzalendo hali inayozidi kuchochea kujilimbikizia fedha za watanzania walalahoi kwa kujinufaisha wenyewe ,hii kasumba ya kuchuma mali pasipo kumuogopa mungu itatufikisha motoni kifo kipo ogopeni kula mali za walipa kodi” alisema Kiswaga
Kwa upande wake Mkaguzi Mkuu wa serikali Patric Mahande amekiri kuwepo kwa udanganyifu wa taarifa ya mapato na mtumizi ya halmashauli hiyo haiendani na miradi inayotekelezwa hususani katika ujenzi wa dampo lililopo eneo la businde Katika manispaa hiyo.
Alisema kuwa gharama za ujenzi huo upo chini ya kiwango ambapo hakilingani na kiasi cha Tsh. Million 15 fedha ambazo zimetumika kwa ajli ya ujenzi huo haingii akilini kwa matumizi yaliyobainishwa katika mradi huo.
Katibu mwenezi wa NRA Rashid amedai kuwa wananchi waache tabia ya kuchagua chama na badala yake wamchague mtu anayefaa katika kuwatekelezea kero zao pamoja na kuwataka wananchi hao kulinda amani na mshikamano uliopo nchini.
0 comments:
Post a Comment