Home » » UDINI WAKEMEWA MKOANI KIGOMA‏

UDINI WAKEMEWA MKOANI KIGOMA‏


Na Mwandishi Wetu, Kigoma.
BARAZA kuu la uhusianao mwema wa kidini Mkoa wa Kigoma umewataka waumini wa dini hizo kudumisha amani, upendo na mshikamano ili kuepusha migogoro na vurugu zinazo sababisha uvunjifu wa amani.
Hayo yalielezwa na viongozi hao jana katika mkutano wa hadhara uliowahusisha waumini wa dini zote na viongozi wa serikali baada ya kumaliza kwa kikao cha pamoja baina ya viongozi hao na Mkuu wa Mkoa Kigoma Luten Kanali Mstaafu Issa Machibya kwa lengo la kuwaonganisha waumini kuwa kitu kimoja na kuondoa tofauti zinzzojitokeza kati yao
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Mwenyekiti wa baraza hilo Shakhe Shabani Guoguo na Katibu Mchungaji Yonasi Katale wa Baraza la Uhusiano mwema wa kidini Mkoani hapa walisema kuwa kutokana na matukio mbalimbali yanayosababisha uvunjifu wa amani imesababisha uongozi wa mkoa kuamua kuitisha kikao cha viongozi wa dini ili kujadili changamoto na kero hizo.
Walisema Matukio yaliyojitokeza hivi karibuni yamesababisha mkuu wa Mkoa Kigoma  na viongozi wa kidini kuunda baraza la uhusiano mwema wa Kidini na kupanga mikakati ambayo itahakikisha waumini ambao watabainika kufanya uchochezi na vurugu kuwajibishwa ipasavyo na baraza hilo.
Aidha akifungua mkutano huo Mkuu wa Mkoa Kigoma Luten Kanal Mstaafu Issa Machibya aliwataka waumini kutekeleza yale mema yanayo hubiriwa katika maeneo yao ya ibada na kuacha chuki zisizo na mafanikio.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa