ILI kukabiliana na
ongezeko la ugonjwa wa kichaa cha mbwa unaowakabili baadhi ya wananchi mara
baada ya kushambuliwa na Mbwa mwenye ugonjwa huo halmashauri ya Manispaa ya
Kigoma Ujiji imeendesha zoezi maalum la kuwachanja mbwa wapatao 900 ili
kuepusha madhara kwa binadamu.
Zoezi
hilo linafanyika kwa mara ya kwanza mkoani humo kwa ushirikiano wa mashirika mbalimbali
ambayo ni pamoja na hifadhi za taifa ya Gombe, mradi wa magonjwa ya wanyama
Serengeti, taasisi ya Jane Goodall na Manispaa hiyo.
Takwimu
za shirika la Afya ulimwenguni WHO linaonyesha kuwa watu 55,000 wanapoteza
maisha kwa mwaka sawa na wastani wa kifo kimoja kila baada ya dakika 10
hususani kwenye nchi za Asaia na Afrika chini ya Jangwa la Sahara ikiwemo
Tanzania.
Dr.
John Shauri ni Daktari wa wanyama katika halmashauri ya Manispaa Kigoma Ujiji ambaye amesema kuwa
Kwa mujibu wa takwimu hizo wanaopata madhara zaidi ni watoto kutokana na tabia
yao kupenda kucheza na wanyama ambao hushambuliwa zaidi kichwani,
usoni au shingo maeneo ambayo ni hatari kwa ugonjwa wa kichaa cha mbwa.
Kwa
upande wake mratibu wa zoezi hilo Dr. Iddi Lipende amesema watu wazima nao
hupata ugonjwa ambapo aslimia 99.9 ya wagonjwa walioonyesha dalili za ugonjwa
huo hufariki dunia kutokana na kutowahi mapema ili kupata tiba
Ameongeza
kuwa Mara baada ya kumalizika kwa zoezi hili wamiliki wa mbwa watalazimika
kulipia kiasi cha sh 5,000 ili kupata huduma lakini kwa waliobahatika kufika
eneo la tukio na kupata chanjo wanaelezea kufurahishwa kwao na zoezi jinsi
lilivyoendeshwa.
0 comments:
Post a Comment