Na Diana
Rubanguka, Kigoma.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda anatarajia
kuwasili leo mkoani Kigoma kwa lengo la kufanya ziara ya kikazi itakayochukua
takribani muda wa siku saba.
Taarifa toka ofisi ya mkuu wa mkoa wa
Kigoma Kanal Mstaafu Issa Machibya kwa waandishi wa habari mkoani humo imesema
waziri Pinda anatarajia kuwasili leo majira ya saa tano asubuhi kwa usafiri wa Ndege.
Katika ziara hiyo atafanya shughuli
muhimu ambapo miongoni mwa shughuli hizo ni pamoja na taarifa ya maendeleo ya
mkoa huo na kuona siraha zilizokamatwa wakati wa operation katika kituo kikuu
cha polisi mkoani kigoma.
Pia atafanya uzinduzi katika ofisi za
wilaya ya Kakonko, Buhigwe, uvinza pamoja na chuo cha kilimo Mubondo,
sanjari na kuweka jiwe la msingi katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya
Uvinza pamoja na bank ya NMB.
Aidha atatembelea miradi mbalimbali
Mkoani kigoma ikiwemo ufugaji wa nyuki pamoja na bwawa la umwagiliaji Nyendara
pamoja na kukagua hifadhi ya situ wa ufugaji nyuki.
Mheshimiwa pinda atatembelea vikundi
mbalimbali vya ujasiliamali pamoja na kufanya mikutano ya hadhara katika maeneo
mbalimbali mkoani humo .
Katika ziara hiyo mheshimiwa
pinda atatembelea pia wilaya sita zilizopo mkoani kigoma ambazo
ni Wilaya ya Uvinza ambayao imetokana na Wilaya ya Kigoma, Wilaya
ya Buhigwe ambayo imetokana na Wilaya ya Kasulu, pamoja na Wilaya ya
Kakonko ambyo imetokana na Wilaya ya Kibondo.
0 comments:
Post a Comment