Na Diana Rubanguka, Kigoma
TIMU ya Mpira wa pete ya
Shule ya Sekondari ya Katubuka iliyopo katika Manispaa ya Kigoma ujiji
imejinyakulia kitita cha sh.500,000 baada ya kutwaa ubingwa wa ligi ya
Wiki ya Usalama Barabarani ikiwa na lengo la kuhamasisha wadau wake
wazingatie sheria na kanuni za Barabara.
Hayo yamebainika jana Mkoani
Kigoma wakati Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama barabarani mkoani
hapa, Abdulqadir Mushi alipokuwa akitaja timu zilizoshiriki na kufanikiwa
kuingia nusu fainali na washindi wa ligi hiyo ambapo timu ya buhanda ikipata
kifuta jasho cha sh.200,000 baada ya kushika nafasi ya pili.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa
Chaneta Mkoa wa Kigoma Amina Malengwa alisema timu
zimeonesha uwezo wao kimashindano katika dakika zote 60,ambapo timu ya mpira wa
pete sekondari ya katubuka iliibuka kwa vikapu 25-21 dhidi ya
sekondari ya Buhanda.
Kwa upande wa walimu wa
timu ya sekondari Katubuka Joanita Emanueli na Siyaleo Sadock mwalimu wa
sekondari Buhanda kwa nyakati tofauti walikiri timu zote kucheza vizuri huku
waonya mashindano kama hayo viongozi watoe tarifa za ushiriki kwa timu husika
mapema ili wajiandae vyema na zawadi ziongezwe.
Kwa nyakati tofauti
wachezaji wa ligi hiyo sekondari ya katubuka Hawa Abdalla na Nuru
Himid walidai timu ya Buhanda ilibebwa na mwamuzi aliyechezesha ligi hiyo
Wakati Bernadeta Bernad Sekondari Buhanda alidai wachezaji wa timu ya sekondari
ya katubuka walikuwa wababe katika ukabaji na kuahidi mwakani watatoa kipigo
cha magori dhidi ya timu hiyo inayoogopwa katika manispaa ya ujiji.
Jambo Leo imebaini
changamoto inayowafanya wachezaji wa timu za mpira wa pete kutosonga mbele
inatokana na urasimu unaofanywa na viongozi wa serikali kutoweka umuhimu katika
sekta hiyo kwa madai haina bajeti yake mbaya zaidi hakuna jitihada
za kuwekea bajeti hatimaye wachezaji wakosa ajira kupitia michezo.
0 comments:
Post a Comment