Rais wa CWT, Gratian Mukoba
MGOGORO wa
walimu wapatao 811 wa Halmashauri ya Ujiji mkoani hapa, umemalizika baada ya
Halmashauri hiyo kuridhia na kuacha mara moja kukata asilimia mbili za
mishahara ya walimu hao kisha kupeleka fedha hizo kwenye Chama cha walimu
Tanzania(CWT).
Taarifa ya
walimu hao kwa vyombo vya habari, iliyosainiwa na Mwenyekiti wa walimu, K.
Sabibi, imesema mgogoro huo ulidumu kwa miaka miwili na nusu na tangu Octoba
,2013, Halmashauri hiyo imekubali kusitisha makato hayo kwa waliokuwa
wamejitosa kupigania haki zao.
‘’Shukrani
kwa viongozi wote hasa mkuu wa wilaya ya Kigoma, Ramadhan Maneno na wasaidizi
wake, waliohakikisha mgogoro huo unamalizika kwa amani’’ imesema taarifa hiyo.
Taarifa hiyo
imemshukuru pia Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Eng.Boniface Nyambele kwa
uelewa wake na kukubali kuchukua hatua za makusudi kwa kusimamisha makato hayo
kwenda CWT yaliyokuwa yakifanyika kinyume cha sheria tangu mwaka 2011.
Wamesema makato
hayo yalikuwa yakifanyika kinyume na sheria ya ajira na mahusiano kazini kama
kifungu cha 61(4) na 5 kinavyoeleza.
‘’Tunapenda
ifahamike kwa walimu wenzetu na umma wa Watanzania kuwa mgogoro uliokuwepo kati
ya walimu wa Kigoma ujiji na mwajiri yaani Mkurugenzi, umekwisha malizika’’
‘’Kwa kuwa
mgogoro huo umekuwa wa muda mrefu na vyombo vya habari vimekuwa vikitoa taarifa,
tunavishukuru sana kwa kazi nzuri kwa kuhabarisha walimu wenzetu na wananchi’’
imesema taarifa hiyo.
Imeeleza
kuwa, kuwepo kwa mgogoro huo kuliathiri utendaji kazi wa walimu hao kwa namna
nyingi ingawa si kwa kiwango kikubwa.
Sanjari na
hayo, walimu hao wamevikumbusha vyama vya wafanyakazi na waajiri, kufanya kazi
kwa kufuata sheria za kazi siyo mazoea na kwamba ikumbukwe kuwa kukata mshahara
wa mwajiriwa bila ridhaa yake ni kosa kama inavyofanya CWT kwa walimu kote
nchini.
chanzo;kalulunga blog
0 comments:
Post a Comment