Mkurugezi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, akiangalia baadhi ya bidhaa katika soko kuu la mkao wa Kigoma. Kulia ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Bw. Bakari Beji. Lengo la zaira ya watendaji wa PSPF mkoani humo ni kukutana na wadau wa Mfuko huo, kuangalia fursa za uwekezaji na kuhamasisha jamii kujiunga katika mpango wa uchangiaji wa hiari (PSPF Supplementary Scheme) ambapo kila mtu anaweza kujiunga na kujipatia mafao bora kwa maisha ya sasa na baadaye.
Ujumbe wa
watendaji wa PSPF pamoja na wale wa Manispaa ya Kigoma Ujiji wakitembelea moja
ya soko. Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu aliongoza ujumbe wa watendaji
wake mkoani Kigoma kwa lengo la kukutana na wadau wa Mfuko huo, kuangalia fursa
za uwekezaji na na kuhamasisha jamii kujiunga katika mpango wa uchangiaji wa
hiari (PSPF Supplementary Scheme)
ambapo kila mtu anaweza kujiunga na kujipatia mafao bora kwa maisha ya sasa na
baadaye.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment