Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
BENKI ya NMB imeendelea kujiimarisha kwa kuzindua tawi jipya mkoani Kigoma, ambalo
lipo eneo la karibu kutoka Barabara ya Bima hadi yalipo majengo ya Shirika la Nyumba
la Taifa (NHC) mkabala na Soko la Mjini Kigoma katika jengo la Lumumba.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi hilo, Meneja wa Kanda ya Magharibi wa Benki hiyo, Abraham Augustino, alisema
tawi hilo limelenga kuhudumia wakazi wa eneo hilo na maeneo ya karibu yanalolizunguka.
Alisema limelenga kutoa huduma bora kwa wateja wake kulingana na mahitaji yao na kuwahakikishia wateja kufikia malengo yao
kibiashara na kiuchumi.
Uzinduzi huo ulifanywa na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Ramadhani Maneno, akiongozana
na Augustino na baadhi ya maofisa wa kanda na wateja na wadau mbalimbali.
Akizungumza
kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo, wakati wa uzinduzi huo mkuu wa wilaya
hiyo, Maneno alisema kuwapo karibu kwa tawi hilo kutachangia maendeleo
kwa wakazi wa Kigoma kiuchumi na ustawi wa
kijamii.
"Tawi hili litafungua milango ya maendeleo kwa wananchi wetu miradi itaendelezwa na
litahudumia wakazi wa eneo hili kwa karibu," alisema Maneno na kuishukuru benki hiyo na kuitakia mafanikio.
Tawi
hilo litatoa huduma za kifedha za viwango vyote na aina zote za mikopo
ya kifedha kwa taasisi, watu binafsi na watumishi wa Serikali bila
usumbufu wala
urasimu, hivyo wakazi wa mkoa huo wametakiwa kutumia fursa hiyo kujiletea maendeleo.
Chanzo:Maaijira
0 comments:
Post a Comment