Na Jonas Kamaleki
Manispaa
ya Uijiji Kigoma imeazimia kuwashirikisha wananchi wake katika mipango
ya maendeleo na kubadli utamaduni uliokuwepo wa kuitegemea Serikali
kuwaletea mipango yake.
Hayo yamesemwa jana Jijini Paris na
Mratibu wa Mpango wa Uendeshaji wa Serikali kwa Uwazi (OGP) Kigoma,
Mhandisi Sultan Ndaliwo wakati wa kufunga Mkutano wa Kilele wa mpango
huo OGP.
Mhandisi
Ndaliwo amesema ushirikishwaji huo utasaidia kutatua changamoto
zinazojitokeza kwa wananchi bila kuwepo kwa ukiritimba kwani masuala
hayo yatakuwa yanajulikana wazi kwa wananchi.
"Nimefurahishwa
na jinsi jiji la Paris linavyowashirikisha wananchi wake katika kupata
maendeleo yao jambo ambalo tutaenda kulitumia Kigoma," alisema Ndaliwo.
Ameongeza
kuwa anaamini Kigoma Ujiji inakwenda kubadilika kutokana na utekelezaji
wa Mpango Mkakati waliojiwekea unatekelzwa ipasavyo.
Kwa
upande wake, Meya wa Manispaa ya Ujiji Kigoma, Sultani Hussein Luhavi
amesema ataenda kuweka mfumo wa utoaji taarifa kwa haraka ambapo
kunatokea tatizo katika eneo lolote ndani ya Manispaa ili lifanyiwe kazi
na wahusika (tracking system).
Amezishauri
Manispaa nyingine zijenge utamaduni wa kuwasilkiliza wananchi na
kuwashirikisha ipasavyo katika mipango ya maendeleo.
"Utendaji wa jinsi hii utabadilisha Manispaa yetu na kuifanya ipige hatua kubwa katika maendeleo," alisema Luhavi.
Luhavi amezitaka Manispaa na Halmashauri za Miji nchini kuiga mfano wa Manispaa ya Ujiji Kigoma ili kuharakisha maendeleo yao.
Halmashauri ya Manispaa ya Ujiji Kigoma ni Kati ya Manispaa 15 duniani zilizojiunga na OGP kama manispaa na si nchi.
Manispaa nyingine zilizojiunga na Mpango huo ni pamoja na Austin
ya Marekani; Bojonegoro, Indonesia; Buenos Aires, Argentina; Elgeyo
Marakwet, Kenya; Jalisco, Mexico; La Libertad, Peru; Madrid, Spain;
Ontario, Canada; Paris, France; Sao Paulo, Brazili; Scotland, Uingereza;
Sekondi-Takoradi, Ghana; Seoul, Korea Kusini and Tbilisi, Georgia.
0 comments:
Post a Comment