Na Magreth Kinabo - Mahakama ya Tanzania
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinad Wambali amesema kwamba mkoa wa Kigoma utapatiwa Mahakama Kuu hivi karibuni,ikiwa ni hatua ya kuwaondolea adha wanaoipata wananchi ya kutafuta huduma ya mahakama hiyo kutoka eneo moja hadi jingine
Kauli hiyoimetolewa tarehe mwishoni mwa wiki iliyopita na Jaji Kiongozi wakati akizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Kibondo kuhusu malengo ya ziara yake katika mkoa wa Kigoma,hivyo aliwataka baadhi ya viongozi na wananchi kuvuta subira.
Jaji Kiongozi , pia alizungumza na baadhi ya viongozi waandamizi wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, wakiwemo baadhi ya watumishi wa Mahakama Kuu kutoka kanda hiyo ambayo inajumuisha mikoa miwili yaani na Tabora na Kigoma.
“Tayari kiwanja kimeshapatikana na eneo la Buhigwe na tenda imeshatangazwa, hivyo mchakato wa ujenzi utaanza hivi, karibuni,”alisema Jaji Kiongozi.
Kiwanja hicho kina ukubwa wa eneo la kilomita za mraba 16,000.
Mkoa huo, unahitaji huduma ya Mahakama Kuu kwa sababu ya kukua kwa idadi ya watu,pia hivi sasa watu wanatoka katika mkoa huo kwenda kufuata huduma za Mahakama Kuu mkoa wa Tabora , pia kukua kwa shughuli za kijamii na kiuchumi.
Jaji Kiongozi aliongeza katika kanda hiyo, wilaya ambazo hazina mahakama za wilaya zitajengewa mahakama kwa kuwa Mahakama ya Tanzania kupitia mpango Mkakati wa Miaka Mitano(2015/16 hadi 2019/20 imejipanga kujenga mahakama kila wilaya, tarafa na kata.
CAPTION YA PICHA
Jaji Kiongozi Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe, Ferdinand Wambali wa akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Mahakama ya Wilaya ya Kasulu mara baada ya kuwasili katika Mahakama hiyo hivi karibuni, wakati alipotembelea Mahakama hiyo na kufanya ukaguzi wa shughuli za utendaji kazi na miundombinu ya Mahakama.
0 comments:
Post a Comment